Mark 5

Isa Amponya Mtu Mwenye Pepo

(Mathayo 8:28-34; Luka 8:26-39)

1 aWakafika upande wa pili wa ziwa wakaingia katika nchi ya Wagerasi. 2 bIsa alipotoka kwenye mashua, mara mtu mmoja mwenye pepo mchafu akatoka makaburini akakutana naye. 3Mtu huyu aliishi makaburini, wala hakuna aliyeweza kumzuia hata kwa kumfunga minyororo. 4Kwa kuwa mara kwa mara alikuwa amefungwa minyororo mikononi na miguuni, lakini akaikata hiyo minyororo na kuzivunja zile pingu miguuni mwake. Hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa na nguvu za kumzuia. 5Usiku na mchana alikuwa makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe.

6Alipomwona Isa kwa mbali, alimkimbilia, akapiga magoti mbele yake. 7 cAkapiga kelele kwa nguvu akisema, “Una nini nami, Isa, Mwana wa Mungu Aliye Juu Sana? Ninakusihi kwa jina la Mungu, usinitese!” 8Kwa kuwa Isa alikuwa amemwambia, “Mtoke mtu huyu, wewe pepo mchafu!”

9Isa akamuuliza, “Jina lako ni nani?”

Akamjibu, “Jina langu ni Legioni,
Legioni maana yake ni Jeshi.
kwa kuwa tuko wengi.”
10Akamsihi Isa sana asiwapeleke nje ya nchi ile.

11Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe lililokuwa likilisha karibu kando ya kilima. 12Wale pepo wachafu wakamsihi Isa wakisema, “Tuamuru twende kwenye wale nguruwe. Turuhusu tuwaingie.” 13Basi Isa akawaruhusu, nao wale pepo wachafu wakatoka, wakawaingia hao nguruwe. Lile kundi lilikuwa na nguruwe wapatao 2,000, nao wote wakateremkia gengeni kwa kasi, nao wakatumbukia ziwani na kuzama.

14Wale watu waliokuwa wakichunga hao nguruwe wakakimbilia mjini na vijijini kueleza yaliyotukia. Watu wakatoka kwenda kuona hayo yaliyokuwa yametukia. 15 eWalipofika kwa Isa, wakamwona yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu legioni akiwa ameketi hapo, amevaa nguo na mwenye akili timamu. Wakaogopa. 16Wale walioyaona mambo hayo wakawaeleza watu wengine yaliyomtokea yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu, na habari za lile kundi la nguruwe pia. 17 fBasi watu wakaanza kumwomba Isa aondoke katika nchi yao.

18 gIsa alipokuwa anaingia kwenye mashua, yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu akamsihi Isa waende pamoja. 19 hIsa hakumruhusu, bali alimwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako ukawaeleze mambo makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokuhurumia.” 20 iYule mtu akaenda zake, akaanza kutangaza katika Dekapoli mambo makuu Isa aliyomtendea. Nao watu wote wakastaajabu.

Mwanamke Aponywa

(Mathayo 9:18-26; Luka 8:40-56)

21 jIsa alipokwisha kuvuka tena na kufika ng’ambo, umati mkubwa wa watu ukamzunguka yeye akiwa hapo kando ya bahari. 22 kKisha mmoja wa viongozi wa sinagogi aliyeitwa Yairo akafika pale. Naye alipomwona Isa, akapiga magoti miguuni pake, 23 lakamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa mahututi. Tafadhali nakusihi, njoo uweke mikono yako juu yake ili apate kupona, naye atakuwa hai.” 24Hivyo Isa akaenda pamoja naye.

Umati mkubwa wa watu ukamfuata, nao watu wakawa wanamsonga.
25 mHapo palikuwa na mwanamke aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili. 26Mwanamke huyu alikuwa ameteseka sana kwa mikono ya matabibu wengi, na kutumia kila kitu alichokuwa nacho. Lakini badala ya kupona, hali yake ilizidi kuwa mbaya. 27Alikuwa amesikia habari za Isa, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, 28 nkwa maana alisema moyoni mwake, “Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitaponywa.” 29 oMara kutoka damu kwake kukakoma, naye akajisikia mwilini mwake amepona kabisa.

30 pGhafula Isa akatambua kuwa nguvu zimemtoka. Akaugeukia ule umati wa watu na kuuliza, “Ni nani aliyegusa mavazi yangu?”

31Wanafunzi wake wakamjibu, “Unaona jinsi umati wa watu unavyokusonga. Wawezaje kuuliza, ‘Ni nani aliyenigusa?’ ”

32Lakini Isa akaangalia pande zote ili aone ni nani aliyemgusa. 33Yule mwanamke, akijua kilichomtokea, akaja, akaanguka miguuni pake akitetemeka kwa hofu, akamweleza ukweli wote. 34 qIsa akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani, upone kabisa ugonjwa wako.”

Isa Amfufua Binti Yairo

35 rAlipokuwa bado anaongea, watu wakafika kutoka nyumbani kwa Yairo. Wakamwambia, “Binti yako amekufa. Kwa nini kuendelea kumsumbua Mwalimu?”

36Aliposikia hayo waliyosema, Isa akamwambia huyo kiongozi wa sinagogi, “Usiogope. Amini tu.”

37 sHakumruhusu mtu mwingine yeyote amfuate isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, nduguye Yakobo. 38 tWalipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi, Isa akaona ghasia, watu wakilia na kuomboleza kwa sauti kubwa. 39 uAlipokwisha kuingia ndani, akawaambia, “Kwa nini mnafanya ghasia na kulia? Mtoto hajafa, bali amelala tu.” 40 vWale watu wakamcheka kwa dharau.

Lakini yeye akawatoa wote nje, akawachukua baba na mama wa yule mtoto, pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao. Wakaingia ndani mpaka pale alipokuwa yule mtoto.
41 wAkamshika mtoto mkono, akamwambia, “Talitha koum!”
Talitha koum ni lugha ya Kiaramu.
(maana yake ni, “Msichana, nakuambia: amka!”)
42Mara yule msichana akasimama, akaanza kutembea (alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili). Walipoona haya, wakastaajabu sana. 43 yIsa akawaagiza kwa ukali wasimweleze mtu yeyote jambo hilo, naye akawaambia wampe yule msichana chakula.
Copyright information for SwhKC